- 145 viewsDuration: 1:08Serikali imewataka Manaibu Kamishna wa Kaunti walioteuliwa hivi karibuni kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na kujitolea ili kuimarisha usalama na uratibu wa huduma za serikali mashinani. Akizungumza jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa mafunzo elekezi kwa maafisa hao, Raymond Omollo alisisitiza kuwa Manaibu Kamishna ni kiungo muhimu kati ya serikali kuu na wananchi katika utekelezaji wa sera na miradi ya maendeleo.