- 408 viewsDuration: 1:22Serikali ya kaunti ya Mandera imesema itahakikisha hakuna mwanafunzi katika kaunti hiyo atakayekosa kuhudhuria masomo kutokana na ukosefu wa karo. Serikali ya kaunti imesema itaendelea kuimarisha programu za ufadhili wa masomo ili kuhakikisha wanafunzi wote, hasa wanaotoka familia zenye uhitaji, wanapata fursa ya kuendelea na elimu bila vikwazo vya kifedha.