Skip to main content
Skip to main content

Maswali yaibuliwa kuhusu mpango wa serikali wa nyumba

  • | KBC Video
    114 views
    Duration: 2:54
    Afisi ya mkaguzi mkuu wa fedha za serikali, imebaini hitilafu kadhaa kwenye mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Kwenye ripoti maalum kwa kamati ya bunge kuhusu fedha za umma, afisi ya mkaguzi mkuu iliangazia changamoto za kifedha na utekelezaji, ambazo hatimaye zinaweza kuathiri ufanisi wa mpango huo. Miongoni mwa maswala yaliyotiliwa shauku, ni pamoja na kesi zinazoendelea mahakamani, hali ya ati ati kuhusu ada za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, pamoja na maswali kuhusu ikiwa Wa-Kenya wana uwezo wa kununua nyumba hizo. Afisi hiyo inayo-ongozwa na Nancy Gathungu, pia imebainisha kuwa swala la umiliki wa ardhi lingali changamoto kuu huku baadhi ya miradi ikiwa kwenye ardhi ambayo haina stakabadhi kamili. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive