- 138 viewsDuration: 1:53Watu wenye ulemavu mjini Kapsabet Kaunti ya Nandi wameelezea changamoto wanazozipitia wakisaka huduma za matibabu, elimu na ajira. Kulingana nao gharama ya afya iko juu mno ikilinganishwa na mahitaji na kipato chao cha kila siku. Sasa wanaitaka serikali kuangazia matatizo hayo ili waishi maisha ya kawaida kama watu wasio na ulemavu.