- 1,439 viewsDuration: 3:12Mbunge wa Kuresoi Alfred Mutai ameachiliwa kwa dhamana baada ya kufikishwa mahakamani kuhusiana na ghasia zilizotokea eneobunge lake na kusababisha watu watatu kujeruhiwa. Mutai alijisalimisha kwa maafisa wa upelelezi Jumatatu jioni na kuzuiliwa kituo cha Polisi cha Nakuru. Mapema leo, vurugu zilishuhudiwa katika kituo hicho huku wafuasi wa mbunge huyo wakitaka aachiliwe au afikishwe mahakamani.