- 927 viewsDuration: 2:42Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o ameibua wasiwasi kuhusu ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma serikalini. Ripoti ya hivi punde ya mwaka wa kifedha wa 2025/2026 inaonyesha kuwa serikali kuu ilitumia zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa safari za nje na ndani ya nchi kwa mwaka mmoja. Ripoti hiyo pia imebaini kuwa baadhi ya miradi ya maendeleo ilianzishwa bila kutengewa fedha katika bajeti. Aidha, deni la taifa liliongezeka hadi shilingi trilioni 13 katika kipindi hicho.