Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki limekuwa likikabiliwa na changamoto za kifedha tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2001.
Changamoto hizo zimeathiri shughuli za bunge hilo, kuchelewesha mishahara ya wabunge na hata kusababisha kusitishwa kwa vikao kwa miezi kadhaa.
Sasa viongozi wa Jumuiya wameidhinisha mfumo mpya wa uchangishaji wa fedha huku maswali yakiibuka kuhusu iwapo utatoa suluhu ya kudumu au kama Bunge la Afrika Mashariki linaelekea kushindwa kutekeleza wajibu wake.
Meluta Ole Tenges alifuatilia mjadala huo kutoka Arusha, Tanzania.