- 491 viewsDuration: 3:02Wakenya katika kaunti mbalimbali wamekosa huduma za matibabu kufuatia mgomo wa wauguzi na wakunga ulioanza jana. Wagonjwa waliofika katika hospitali za umma katika kaunti za Kericho, Machakos, Kisumu, Kisii na Embu walilazimika kurejea nyumbani baada ya kukosa huduma kutokana na kutokuwepo kwa wauguzi. Viongozi wa wauguzi wanailaumu Baraza la Magavana kwa kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo, hali iliyochangia kuanza kwa mgomo huo. Chrispine Otieno ana taarifa zaidi.