Skip to main content
Skip to main content

Mkutano wa faragha wa kutatua mgomo wa wafanyakazi wa viwanja vya ndege waendelea

  • | Citizen TV
    3,503 views
    Duration: 29s
    Maafisa wakuu wa Wizara ya Uchukuzi, wanachama wa Muungano wa Wafanyakazi wa Viwanja vya Ndege (KAWU), Tume ya Kuratibu Mishahara pamoja na Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Nchini (COTU) kwa sasa wanaendelea na mkutano wa faragha hapa Nairobi, katika juhudi za kutatua mgomo huo uliodumaza usafiri katika viwanja vya ndege humu nchini. Mkutano huo ulioanza jana jioni umeendelea leo na hadi sasa ungali unaendelea.