- 432 viewsDuration: 2:58Chuo Kikuu cha Moi sasa kinapanga kuwafuta kazi wafanyakazi zaidi ili kupunguza mzigo wa madeni unaoendelea kukisambaratisha. Akizungumza mbele ya Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa leo, Kaimu Naibu Chansela wa chuo hicho, Prof. Kiplagat Kotut, amesema chuo hicho kinaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, huku kikiwa na upungufu wa bajeti wa zaidi ya shilingi bilioni 8 na madeni yanayofikia shilingi bilioni 10.