- 9,608 viewsDuration: 3:29Mahakama Kuu mjini Naivasha imemwachilia huru mshukiwa mmoja kati ya washukiwa tisa wa mkasa wa moto uliosababisha vifo vya wanafunzi kumi na sita katika Shule ya Utumishi, Gilgil. Hatua hiyo imefuatia upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka mwanafunzi huyo. Mwanafunzi huyo amekabidhiwa wazazi wake huku washukiwa waliosalia wakizuiliwa hadi Ijumaa ambapo kila mmoja anatarajiwa kufunguliwa mashtaka kumi na sita ya mauaji katika Mahakama Kuu ya Nairobi. Mary Muoki anaripoti kuwa kesi hiyo imehamishiwa Nairobi kwa sababu za usalama.