- 8,306 viewsDuration: 2:49Msongamano mkubwa wa magari umeendelea kushuhudiwa katika makutano ya Barabara ya Valley Road na ile kutoka Mahakama ya Milimani kuelekea Barabara ya Kenyatta Avenue jijini Nairobi. Hali hiyo inatokana na ujenzi unaoendelea wa barabara ya juu inayolenga kuunganisha eneo la Upper Hill na katikati mwa jiji. Walioathirika zaidi hususan wamiliki wa magari ya usafiri wa umma wamelalamikia msongamano huo wakisema umezidi na kuitaka serikali kutoa njia mbadala za kupunguza athari kwa watumiaji wa barabara.