Skip to main content
Skip to main content

Msongamano wa warundi kutafuta stakabadhi za usafiri

  • | Citizen TV
    11,560 views
    Duration: 3:19
    Msongamano mkubwa ulishuhudiwa katika Ubalozi wa Burundi nchini Kenya, ambapo raia wa nchi hiyo walifurika kutafuta stakabadhi za usafiri kurejea kwao. Warundi hao walirundikana katika ofisi za ubalozi huo kutwa nzima, siku moja baada ya makataa yaliyowekwa na serikali kwa raia wa kigeni wasio na vibali nchini kuondoka kukamilika. Hata hivyo, agizo hilo limeibua wasiwasi miongoni mwa raia hao, huku baadhi wakikabiliwa na changamoto ya kupata stakabadhi muhimu za safari. Ben Kirui ana taarifa zaidi kuhusu agizo hilo.