- 2,051 viewsDuration: 2:58Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amepuuzilia mbali uzito wa tatizo la magenge ya wahuni nchini, akisisitiza kuwa limezidishwa na siasa na wanasiasa. Hata hivyo, ameagiza polisi na maafisa wa upelelezi kuanza rasmi msako dhidi ya magenge hayo, akisisitiza kuwa Wakenya wanaunga mkono vita dhidi ya wahuni. Murkomen alikuwa akizungumza alipozindua rasmi mfumo mpya wa kidijitali wa kuchapisha vyeti vya rekodi za uhalifu kwa Wakenya.