- 7,320 viewsDuration: 2:25Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen sasa anadai kwamba kuna njama ya kufufua na kudhamini kundi lililopigwa marufuku la Mungiki, kwa lengo la kutekeleza uhalifu dhidi ya wafanyikazi wa serikali na wafuasi wa rais William Ruto katika eneo la Mlima Kenya. Aidha, waziri wa Ulinzi Soipan Tuya amemkashifu Gachagua kwa kuendeleza uhasama na chuki miongoni mwa jamii nchini, huku akirai wakenya kukataa kugawanywa kikabila.