- 5,036 viewsDuration: 1:58Waziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, amemuonya kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, kuhusu matamshi anayodai ni ya uchochezi na yanayochochea mgawanyiko nchini. Murkomen amemkashifu Gachagua kwa kuwataja viongozi wa Mlima Kenya wanaounga mkono serikali kuwa wasaliti. Waziri huyo amesema amewaagiza maafisa wa usalama kufuatilia kwa karibu matamshi ya Gachagua na kuchukua hatua za kisheria iwapo itabainika kuwa yamekiuka sheria.