- 1,202 viewsDuration: 3:06Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amewaonya watu wanaomiliki silaha haramu katika eneo la Angata Barrikoi, kaunti ya Transmara, kuzisalimisha mara moja. Agizo hilo limetolewa kufuatia mkutano uliofanyika baada ya kuzuka kwa mapigano mapya yaliyodumu kwa takriban siku tatu katika eneo hilo. Haya yanajiri huku afisa mmoja wa usalama akiuawa katika mzozo wa hivi karibuni na hali ya usalama ikiendelea kusalia tete.