- 7,940 viewsDuration: 1:09Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amezitaka shule zote nchini kufunga kamera za CCTV ili kusaidia kufuatilia mienendo ya wanafunzi na kuimarisha usalama shuleni. Akizungumza katika hafla ya shukrani iliyofanyika katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Kipsigis, kaunti ya Kericho, Murkomen alisema kuwa ukaguzi wa mara kwa mara wa picha za CCTV katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Utumishi, Gilgil, huenda ungezuia mkasa wa moto uliosababisha vifo vya wanafunzi 16. Waziri huyo alisisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuimarisha usalama wa wanafunzi na kuzuia matukio ya majanga katika taasisi za elimu.