- 1,178 viewsDuration: 2:41Muungano wa upinzani umesisitiza kuwa utamtaja mgombea mmoja wa kuwania urais dhidi ya Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa chama cha People’s Renaissance Movement (PRM), viongozi hao wamekitaja chama hicho kama nguvu mpya katika safari ya kumwondoa Rais Ruto mamlakani. Aidha, viongozi hao wamemshutumu Msajili wa Vyama vya Kisiasa kwa kukwamisha usajili wa chama cha Linda Mwananchi.