- 1,372 viewsDuration: 2:28Kesi ya mauaji ya Rex Masai sasa inachukua mwelekeo mpya baada ya maafisa wa Independent Policing Oversight Authority kudai kuwa Idara ya Polisi inasambaratisha juhudi zao za kutafuta haki kwa marehemu. Kwa upande wao, mawakili wanaowakilisha Polisi wanasisitiza kuwa uchunguzi ufanywe kwa kutumia kanda za CCTV ili kubaini kilichotokea, pamoja na uchunguzi wa risasi, maganda ya risasi na bunduki iliyotumika, hatua ambayo imehusisha mshukiwa mkuu anayedaiwa kuwa afisa wa polisi Isaiah Muragiri katika eneo la tukio.