Skip to main content
Skip to main content

Mvutano wazidi bungeni kuhusu mswada wa fedha 2026

  • | Citizen TV
    1,637 views
    Duration: 3:18
    Vuta nikuvute kuhusu mswada wa fedha wa mwaka 2026 imeendelea leo bungeni huku wabunge wanaoegemea upande wa serikali na wale wa upinzani wakikabiliana kuhusu baadhi ya mapendekezo ya mswada huo. Wabunge wanaoegemea upande wa serikali wakiongozwa na Kinara wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah wamepuuzilia mbali madai kwamba ushuru wa mitumba na simu umeongezwa, huku wale wa upinzani wakisisitiza kuwa ushuru huo upo na kuapa kupinga mswada huo utakapowasilishwa kwa kura.