- 6,983 viewsDuration: 1:15Mzazi mmoja wa mwanafunzi wa shule ya upili ya Utumishi Academy ni miongoni mwa watu wanne walioaga dunia katika ajali mbili tofauti zilizotokea eneo la Gilgil, kaunti ya Nakuru. Mama huyo alikuwa akisafiri na mumewe kuelekea shule ya wasichana ya Utumishi Academy baada ya kuarifiwa kuhusu mkasa wa moto uliotokea shuleni hapo mapema leo. Wawili hao walikuwa wameabiri gari la kibinafsi lililogongana ana kwa ana na trela. Mwili wa mama huyo ulipelekwa katika makafani ya Hospitali ya Gilgil, huku mumewe akiwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Nakuru.