Skip to main content
Skip to main content

Mwanaharakati Halima Ngache azuiliwa hadi wiki ijayo

  • | Citizen TV
    4,608 views
    Duration: 2:53
    Mwanaharakati Halima Ngache ataendelea kuzuiliwa hadi wiki ijayo baada ya kufikishwa mahakamani Nairobi leo kwa tuhuma za kuchapisha taarifa kuhusu safari ya ndege ya Rais William Ruto katika mtandao wa X. Halima, ambaye alikamatwa nyumbani kwake Kadzandani, Mombasa, Jumanne asubuhi, alikana mashtaka hayo katika Mahakama ya Milimani. Tukio hilo limejiri huku familia yake ikilalamikia kutoweka kwake na kueleza kuwa ilihangaika kumtafuta kwa zaidi ya saa 24 bila kujua alikokuwa, kama anavyoarifu Francs Mtalaki.