Skip to main content
Skip to main content

Mwanamke abakwa na watu sita kijijini Bula Medina, Garissa

  • | Citizen TV
    27,624 views
    Duration: 2:43
    Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 28 analilia haki baada ya kubakwa na genge la watu sita katika kijiji cha Bula Medina viungani mwa mji wa Garissa wikendi iliyopita. Kulingana na mwanamke huyo, genge hilo lilivunja mlango wa nyumba yao mwendo wa saa nane usiku na aliamurishwa kupanda kwa pikipiki mbele ya mumewe kisha kupelekwa kwenye kichaka na kutendewa unyama huo . Majirani waliojitokeza kumuokoa walishambuliwa kwa mapanga na kujeruhiwa na wahalifu hao. Kamanda wa polisi kaunti hiyo Samson Chelugo anasema wamefanikiwa kuwakamata washukiwa watano ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo.