Skip to main content
Skip to main content

Mwanamke akamatwa kwa kudaiwa kumuua mumewe Nakuru

  • | Citizen TV
    4,777 views
    Duration: 1:15
    Polisi kaunti ya Nakuru wamemkamata mwanamke anayedaiwa kumuua mumewe kwa kumchoma kisu nyumbani kwao katika eneo la Rongai. Mwanamke huyo wa miaka 37 anadaiwa kumchoma kisu mumewe, Alphonse Ochieng, mwenye umri wa miaka 27, kufuatia mzozo wa kinyumbani. Majirani wameripoti kuwa wanandoa hao walikuwa wakikumbwa na migogoro ya mara kwa mara kwa muda sasa. Mshukiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho Jumatatu, huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Nakuru Level 5 Annex ukisubiri uchunguzi.