- 2,077 viewsDuration: 2:48Hofu imeendelea kutanda katika eneo la Lolgorian, Transmara Kusini, kaunti ya Narok, baada ya vurumai kuzuka kati ya maafisa wa polisi na wenyeji. Makabiliano hayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja, huku wengine kadhaa, wakiwemo maafisa sita wa polisi, wakijeruhiwa. Zogo hilo la Ijumaa lilizuka kufuatia kukamatwa kwa wachimba dhahabu katika eneo la Mlima Kilima Pesa. Chrispine Otieno ana taarifa zaidi kutoka Narok.