- 1,385 viewsDuration: 1:09Gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia, George Natembeya, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuzingatia mazungumzo yenye heshima na siasa za hoja wanapotwaa majukwaa ya kisiasa. Natembeya akisema kuwa matumizi ya lugha ya chuki, kejeli na dharau yanachochea migawanyiko nchini. Akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika kaunti ya Trans Nzoia, gavana huyu pia amewalaumu viongozi anaosema wanatumia lugha ya kuchochea na kuwagawanya wakenya.