Tume ya Uwiano na Utangamano Nchini (NCIC) imesema itawapiga darubini viongozi wa kisiasa ili kudhibiti semi za uchochezi ambazo zimekuwa zikienea katika majukwaa mbalimbali ya kisiasa.
Akizungumza baada ya kuhudhuria ibada katika kaunti ya Nairobi, mwenyekiti wa tume hiyo Kepha Nyamweya aliwaonya Wakenya dhidi ya kutumia vibaya uhuru wa kujieleza kwa kueneza chuki.
Kauli hiyo imejiri huku viongozi mbalimbali wakiendelea kupaza sauti kuhusu ongezeko la semi za chuki, hasa katika mikutano ya kisiasa.