- 16,930 viewsDuration: 2:43Waziri wa Afya Aden Duale amejipata matatani kufuatia matamshi yake ambayo yalionekana kushambulia jamii ya Wakikuyu nchini. Tume ya Uwiano na Utangamano nchini, NCIC sasa ikianzisha uchunguzi kuhusu matamshi hayo ya jumanne wiki iliyopita katika hafla moja kaunti ya Mandera. Kupitia kwa taarifa, NCIC imeahidi kuzamia uchunguzi wa kina dhidi ya waziri Duale ambaye sio mara ya kwanza kujipata na ulimi telezi.