Skip to main content
Skip to main content

Ndindi Nyoro aomba msamaha kwa kukosa kura ya Mswada wa Fedha.

  • | Citizen TV
    4,342 views
    Duration: 1:20
    Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amejitetea baada ya maswali kuibuka kuhusu kutoshiriki kwake katika upigaji kura bungeni wakati wa kupitishwa kwa Mswada wa Fedha wa mwaka 2026. Akizungumza na wanahabari, Nyoro amesema alishiriki katika mchakato mzima wa kushinikiza marekebisho ya baadhi ya vipengee vya mswada huo na kuwaomba Wakenya msamaha kwa kutoshiriki katika kura ya mwisho. Mbunge huyo pia amesema kuwa baada ya wiki tatu atatangaza mwelekeo wake wa kisiasa.