- 15,492 viewsDuration: 3:13Mwanafunzi wa mwisho kwenye mkasa wa moto wa Utumishi Girls Academy amezikwa nyumbani kwao eneo la Ruai hapa Nairobi. Neema Wairimu Murigi, aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha nne, alipewa mkono wa buriani kwenye hafla ya mazishi iliyogubikwa na huzuni na majonzi. Wazazi wake, dada zake na wanafunzi wenzake walioshiriki hafla hiyo walishindwa kujizuia walipokuwa wakitoa heshima zao za mwisho.