Skip to main content
Skip to main content

Ngunjiri Wambugu awasihi upinzani kuzingatia sera kuelekea 2027

  • | Citizen TV
    485 views
    Duration: 1:32
    Aliyekuwa mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu, amevitaka vyama vilivyoko upinzani kuendesha kampeni zao bila ya kuvidharau vingine vilivyoko ndani ya muungano huo, huku akionya hakuna chama kilichojinadi kikamilifu kokote. Akizungumza saa chache kabla ya Kinara wa DCP Rigathi Gachagua kuongoza mikutano ya hadhara kwenye eneo bunge hilo adhuhuri ya leo, Wambugu amemtaka Gachagua kukumbatia siasa za Sera na kutupilia mbali kejeli kwa wasio wafuasi wa chama chake.