Skip to main content
Skip to main content

Njuguna Ndung'u amtuhumu Ruto kuingilia taasisi za umma

  • | Citizen TV
    4,843 views
    Duration: 3:21
    Rais William Ruto anapojiandaa kutoa hotuba kuhusu hali ya taifa, aliyekuwa Waziri wa kwanza wa Hazina ya Kitaifa katika utawala wake, Profesa Njuguna Ndung'u, amemtuhumu kwa kuingilia uhuru wa taasisi za umma. Akizungumza katika kongamano la maendeleo nchini Sweden, Profesa Ndung'u alisema kudhoofishwa kwa taasisi za umma kumekuza ufisadi na kuathiri juhudi za kuwawezesha wananchi wa kawaida kiuchumi. Alitoa kauli hiyo huku Rais Ruto akitarajiwa kueleza mafanikio ya serikali yake katika hotuba yake kwa taifa.