- 4,677 viewsDuration: 54sKampuni ya habari ya NTV Uganda pamoja na vituo vyake vingine ililazimika kusitisha matangazo kufuatia uvamizi wa kijeshi ulioagizwa na Mkuu wa Majeshi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba. Jenerali Muhoozi, ambaye ni mwana wa Rais Yoweri Museveni, aliamuru hatua hiyo baada ya shirika hilo kuchapisha habari zilizoikosoa serikali na taasisi za usalama nchini humo. Hatua hiyo iliathiri shughuli katika makao makuu ya Nation Media Group Uganda yaliyoko Namuwongo jijini Kampala, pamoja na shughuli za Spark TV na gazeti la Daily Monitor. Viongozi wa upinzani na makundi ya kutetea haki za binadamu wameikosoa hatua hiyo wakisema inalenga kudhoofisha uhuru wa vyombo vya habari.