Kwa miaka mingi, eneo la kati halikuwahi kushuhudia maandamano ya kiwango kikubwa na hata yale yaliyoshuhudiwa hayakuwahi kwa njia yoyote kuchangia uvamizi wa biashara na vitega uchumi tofauti vya wakazi. Ila mwaka huu wa 2025, matukio mapya yalishuhudiwa eneo hili, Ikiwa ni pamoja na mali kuporwa na vifo vikishuhidiwa wakati wa maandamano ya juni 25 na julai 7. Na kama anavyoangazia sasa Kamau Mwangi, Nyeri ni mojawapo ya kaunti zilizoshuhudia matukio haya, ikiwa ni pamoja na pia matukio ya kuvamiwa kwa wanahabari na kuafikiwa kwa rekodi ya binadamu wa kwanza duniani kuukumbatia mti kwa muda mrefu duniani.