Skip to main content
Skip to main content

Nyoro, Karua walalamikia utekaji na kukandamizwa kwa wanahabari

  • | Citizen TV
    2,744 views
    Duration: 1:39
    Kinara wa chama cha PPK Ndindi Nyoro ameibua wasiwasi kuhusu ripoti za utekaji nyara na ushuru wa kiholela akiitaka serikali kuheshimu katiba na kuhakikisha mazingira bora kwa Wakenya na biashara. Akizungumza alipokutana na wanachama wa PPK kutoka Homa Bay na maeneo mengine nchini, Nyoro amesema idara za usalama zinapaswa kuheshimu sheria na haki za wananchi. Kauli yake ikiungwa mkono na kinara wa chama cha PLP Martha Karua ambaye alishutumu kukandamizwa kwa wanahabari. Karua alikuwa akizungumza na viongozi wanawake kutoka Embu katika kanisa la St. Paul’s ACK mjini humo..