- 6,583 viewsDuration: 1:35Kinara wa ODM Dkt. Oburu Oginga amesema yuko salama na anaendelea kupokea matibabu jijini London, Uingereza, kwa ushauri wa madaktari wake. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Oburu amesema matibabu hayo yamesababishwa na changamoto zinazohusiana na umri. Amesema manaibu wake, Gavana wa Kisii Simba Arati na Gavana wa Mombasa Abdullswamad Shariff Nassir, watashikilia uongozi wa ODM hadi atakaporejea nchini. Haya yanajiri huku ODM ikitangaza maadhimisho ya mwezi wa Baba, kwa ajili ya kuadhimisha na kukumbuka maisha ya aliyekuwa kinara wa chama hicho, marehemu Raila Odinga.