- 4,104 viewsDuration: 2:42Viongozi wa ODM sasa wanasema kuwa wanasiasa wa Linda Mwananchi watabeba jukumu wenyewe, wakidai wamekuwa wakichochea vurugu katika mikutano yao ya kisiasa. Wakiongozwa na mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga, viongozi wa ODM wakijumuisha waziri wa kawi Opiyo Wandayi wamesema ni kinaya kuwa mrengo huo hushambuliwa tu katika mikutano eneo la Nyanza, akisema ni njama ya kuipaka tope ODM. Laura Otieno na taarifa hii kwa kina.