Skip to main content
Skip to main content

ODM yapuuza madai ya mpasuko ndani ya chama

  • | Citizen TV
    2,300 views
    Duration: 1:46
    Viongozi wa chama cha ODM wamepuuza madai ya kuwepo kwa mpasuko ndani ya chama hicho, wakisisitiza kuwa tofauti za kisiasa zinazojitokeza katika baadhi ya maeneo ni sehemu ya demokrasia ya chama na haziwezi kutikisa msingi wake. Wakizungumza katika Kongamano la Vijana wa ODM mjini Busia, viongozi hao walikiri kuwepo kwa dalili za siasa za ubabe katika baadhi ya maeneo lakini wakasema uongozi wa chama utashughulikia tofauti hizo. Viongozi hao pia wameahidi kuwa ODM itaendelea kuimarisha na kulinda ngome zake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.