- 259 viewsDuration: 1:51Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya amekana madai kuwa serikali inabuni sheria zaidi ili kudhibiti vyama vya ushirika nchini. Akizungumza huko Mombasa kwenye kongamano la Muungano wa Vyama vya Ushirika barani, Oparanya amekashifu ubadhirifu wa fedha katika Muungano wa Vyama vya Ushirika (KUSCCO) pamoja na kufungwa kwa Chama cha Ushirika cha Metropolitan. Mkurugenzi wa Uhariri katika kampuni ya Royal Media Services Linus Kaikai amewataka wakuu wa vyama vya ushirika kuwekeza kwenye teknolojia katika shughuli zao ili kukabiliana na changamoto ya taarifa za kupotosha.