- 1,977 viewsDuration: 2:54Kuna uwezekano kwamba wakazi wa Nyeri wamekuwa wakila nyama ambayo haijakaguliwa. Hii ni baada ya asasi za usalama mjini humo kunasa zaidi ya kilo mia tano za nyama ya ng’ombe kwenye boma moja eneo la Measure viungani mwa mji huo. Katika operesheni hiyo ya kuwasaka wezi wa mifugo, watu saba wamekamatwa kwa kuendesha kichinjio haramu, huku mihuri bandia, pikipiki moja na magari matatu yanayokisiwa kuhusika kusafirisha nyama hiyo yakipatikana.