Skip to main content
Skip to main content

Operesheni ya polisi Trans Nzoia

  • | Citizen TV
    477 views
    Duration: 1:43
    Gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia ameshutumu vikali oparesheni inayoendelezwa na kitengo maalum cha polisi katika kaunti hiyo, akisema inakiuka haki za kibinadamu kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi. Amesema pia oparesheni hiyo inalenga vijana, wakiwemo wale wanaoikosoa serikali. Haya yanajiri juma moja tu baada ya oparesheni hiyo kuanza rasmi katika Kaunti ya Trans Nzoia, ambapo vijana zaidi ya mia mbili wametiwa mbaroni kwa madai ya kuwa miongoni mwa magenge yanayowatatiza wakazi wa kaunti hiyo. Akizungumza katika eneo la Chebukaka, eneobunge la Saboti, kiongozi huyo ameitaka idara ya polisi kutojiingiza katika siasa na kuepuka kutumika kuwanyanyasa wananchi.