Skip to main content
Skip to main content

Police Bullets yaanza vyema kampeni ya kufuzu Klabu Bingwa Afrika

  • | Citizen TV
    388 views
    Duration: 39s
    Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Kenya, Police Bullets, wameanza vyema katika mechi za kufuzu kwa michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika baada ya ushindi wa bao 2-1 dhidi ya mabingwa wa Tanzania, Simba Queens. Police Bullets walikuwa timu bora katika dakika za mwanzo za mechi na walizawadiwa kwa bao lililofungwa na Faith Moraa Mboya katika dakika ya 17 ya mechi. Simba Queens walirudi kwa nguvu, lakini Polisi walishikilia uongozi wa 1-0 kufikia wakati wa mapumziko. Katika kipindi cha pili, shinikizo la Simba Queens lilizaa matunda walipopata bao la kusawazisha kupitia kwa Senaf Denise Wakuma katika dakika ya 70. Mchezaji mpya Martha Amnyolet alifunga bao hilo la ushindi zikiwa zimesalia dakika kumi kucheza. Simba Queens walishinda mechi yao ya kwanza 2-0 dhidi ya Top Girls Academy. Police Bullets wako nafasi nzuri ya kuongoza Kundi C ikiwa watapata pointi dhidi ya Top Girls Academy katika mechi yao ijayo.