- 360 viewsDuration: 59sPolisi wa trafiki na maafisa wa NTSA wamehimizwa kujitahidi kuhakikisha madereva na waendeshaji pikipiki walioko barabarani wote wamehitimu kama njia ya kuzuia visa vya ajali nchini. Akizungumza alipotoa ufadhili wa kutoa mafunzo ya uendeshaji magari na pikipiki South C, mwakilishi wadi wa South C Abbas Khalif amesema kuna haja ya kuwalinda wakenya barabarani kwa kuhakikisha madereva wamehitimu . Vijana 300 kutoka wadi sita za South C watanufaika na ufadhili huo .