- 2,862 viewsDuration: 1:19Maafisa wa polisi wanachunguza kifo tata cha mwanafunzi wa taasisi ya masomo ya Kiislamu ya Makindu, aliyefariki kwa njia tata wiki jana. Familia ya Ahmed Amir Rosa, mwenye umri wa miaka 28, inadai haki baada ya upasuaji wa maiti kuonyesha kuwa kijana wao alikuwa na majeraha mabaya na alifariki kutokana na kupigwa, licha ya taasisi hiyo kudai kuwa aliugua na kufariki. Mashirika ya kutetea haki sasa yanataka uchunguzi kufanywa, yakidai taasisi hiyo imehusishwa na visa vya dhuluma dhidi ya wanafunzi. Polisi nao wanasema wanamsaka mmiliki wa taasisi hiyo, ambaye aliripotiwa kutoweka baada ya kisa hicho.