- 4,048 viewsDuration: 2:18Polisi katika eneo la Koingeren, Kaunti ya Kericho, wanachunguza kisa ambapo wanafunzi wawili wameuawa na miili yao kumwagiwa kemikali kuteketezwa. Kati ya wawili hao, mwanafunzi wa kike mwenye miaka kumi na sita anaaminika kubakwa na kunyongwa kabla ya kuchomwa kwa kemikali. Wawili hao wanaaminika kutoweka katika njia tata siku sita zilizopita, kama Bonface Barasa anavyotuarifu.