- 1,347 viewsDuration: 2:46Kwa mara nyingine tena, polisi mjini Karatina walilazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji baada ya maandamano ya amani yaliyokuwa yakiendelea kutibuka katika dakika za mwisho. Hali hiyo ilisababisha michezo ya paka na panya kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi waliokuwa wakifanya doria, ambapo watu watatu walikamatwa. Wakati huo huo, mji wa Nyeri ulisalia na utulivu mchana kutwa huku shughuli za biashara zikiendelea kama kawaida.