Skip to main content
Skip to main content

Radio Citizen yashirikiana na waumini katika ibada Rongo

  • | Citizen TV
    522 views
    Duration: 1:11
    Radio Citizen imezuru eneo la Rongo, kaunti ya Migori, kwa ibada ya Jumapili ambapo mamia ya waumini walijumuika na kupata fursa ya kukutana na watangazaji wao wanaowapenda. Ziara hiyo iliwaleta pamoja wasimamizi na watangazaji wa Radio Citizen waliohudhuria ibada katika Kanisa la Trumpet of God. Hii ikiwa ni dhamira ya Radio Citizen kuendelea kushirikiana na jamii mashinani kupitia vipindi vyake. Askofu wa kanisa hilo, Pius Achilla, ameipongeza Royal Media Services kwa kuendelea kufikia jamii na kudumisha uhusiano wa karibu na wasikilizaji.