- 6,496 viewsDuration: 3:03Raia wa kigeni walio nchini bila stakabadhi au vibali vya kufanya biashara wamepewa siku 90 zaidi kujipanga na kuhakikisha wako nchini kihalali. Taarifa ya serikali iliyotolewa na Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed imekuwa afueni kwa baadhi ya raia hao, ambao wengi walikuwa wameanza kuondoka nchini. Hata hivyo, baadhi ya raia wa kigeni waliendelea kufika katika balozi zao kutafuta hati za usafiri za kurejea makwao. Mrundiko mkubwa wa raia wa Burundi ulionekana kwa siku ya pili mfululizo, huku wakitafuta namna ya kuondoka nchini.