Skip to main content
Skip to main content

Ruto aanza ziara Wajir, aongoza uzinduzi wa miradi ya maendeleo

  • | Citizen TV
    1,251 views
    Duration: 1:46
    Rais William Ruto ameanza rasmi ziara ya siku tatu katika kaunti ya Wajir, ambapo anazindua miradi mbalimbali ya maendeleo kabla ya kuongoza sherehe za Madaraka Day zitakazofanyika Jumatatu. Rais ameanza ziara hiyo ya maendeleo mjini Habasweni kwa kufungua mradi wa usambazaji umeme, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za nishati katika eneo hilo. Viongozi walioandamana naye wamesema eneo la Kaskazini Mashariki linaunga mkono azma yake ya kuwania muhula wa pili ofisini. Wakati huohuo, Katibu katika Wizara ya Usalama wa Ndani Raymond Omollo amesema kuwa maandalizi ya sherehe za Madaraka Day yamekamilika kikamilifu.